Ni jukumu la Bodi ya Tumbaku Tanzania kuwa na orodha ya vituo vyote vya kufungia na kuuzia tumbaku vitanavyotumika wakati wa masoko ya tumbaku. Kila chama cha Msingi kinawajibika kuomba usajili wa vituo vya kufungia na kuuzia tumbaku.
Kwa upande wa vituo vikuu vya kuuzia tumbaku, mnunuzi husika anawajibika kuomba usajili wa vituo vitakavyotumika kuuzia tumbaku. Usajili wa vituo vya kufungia na kuuzia tumbaku hufanyika kila msimu wa masoko ya tumbaku. Mara nyingi kuanzia mwezi Machi mpaka Aprili ya mwaka wa kalenda.
Namna ya kuomba usajili
Maombi hufanyika kwa njia ya mtandaoni kupitia kiungo hiki: ATMIS. Bodi inapopokea maombi, ukaguzi wa eneo unafanyika na ikiridhika na hali ya eneo hilo basi Bodi hutoa Hati ya usajili.