Katika kutekeleza majukumu yake, Bodi ya Tumbaku Tanzania imepewa mamlaka ya kisheria yafuatayo:

  1. Kusajili au kutoa leseni kwa wakulima, wauzaji na wasindikaji wa tumbaku,
  2. Kutoa leseni kwa wanunuzi, wauzaji na wasindikaji  wa tumbaku,
  3. Kutoa leseni kwa ajili ya kusafirisha au uingizaji wa tumbaku kutoka au katika Tanzania
  4. Kuteua wakaguzi kwa ukaguzi wa maeneo ya tumbaku, na kitu chochote ambacho kinaweza kukaguliwa kwa ajili ya kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya sheria.