Idara ya Fedha na Utawala ina majukumu yafuatayo:

  • Kumushauri Mkurugenzi Mkuu juu ya masuala yanayohusu mipango na usimamizi wa fedha, rasilimali watu na mali za Bodi;
  • Kusimamia mwenendo wa masuala ya fedha na shughuli za bodi;
  • Kuimarisha usimamizi sahihi wa fedha na hesabu za Bodi;
  • Kuratibu maandalizi na matayarisho ya bajeti ya mwaka ya bodi;
  • Kuelekeza na kusimamia maandalizi ya taarifa za fedha za mara kwa mara na kuhakikisha zinawasilishwa kwa mamlaka husika kulingana na kanuni;
  • Kuimarisha matumizi bora ya mapato ya Bodi katika ununuzi na utoaji wa huduma na vifaa;
  • Kufuatilia upatikanaji wa fedha kutoka vyombo husika na kusimamia matumizi ya bajeti ya Bodi na kwa kila idara;
  • Kuimarisha ukaguzi wa taarifa za fedha za Bodi kwa wakati;
  • Kuandaa na kutafsiri sera zinazokuhusiana na huduma za kijamii za wafanyakazi, uboreshaji wa nguvu kazi, ujira na mishahara, mafao na masula mengine yanayohusu ustawi wa wafanyakazi;
  • Kuimarisha rasilimali watu na ujuzi unaohitajika katika ngazi zote za idara/sehemu.