Ili kuendeleza na kusimamia sekta ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia ofisi ya Mkurugenzi Mkuu inatekeleza majukumu yafuatayo:

  • Kudumisha na kukuza ufanisi, na utawala bora wa Bodi;
  • kuwajibika kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya utekelezaji wa maamuzi yake;
  • Kusimamizi maendeleo endelevu na mapitio ya dira, malengo na sera za bodi;
  • Kuandaa na kutekeleza sera za taasisi na sera za usimamizi kwa ajili ya kuendesha bodi na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba bodi inafanya kazi ndani ya bajeti ya matumizi iliyoidhinishwa;
  • Kuishauri Bodi ya Wakurugenzi juu ya uteuzi wa wakurugenzi na wakuu wa vitengo;
  • Kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati wa Bodi;
  • Kuishauri serikali juu ya masuala yote yanayohusiana na sekta ya tumbaku na kupendekeza mipango mikubwa ya sera;
  • Kuiwakilisha bodi katika mikutano ya tumbaku ya ndani ya nchi na ya kimataifa;
  • Kukuza, kuanzisha na kuratibu ushiriki au ushirikiano wa sekta ya tumbaku ya Tanzania katika sekta ya tumbaku ya kikanda na kimataifa;
  • Kukuza uhusiano mzuri miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika mengine.