Ili kuendeleza na kusimamia sekta ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Idara ya Uendelezaji zao na Huduma za Usimamizi inatekeleza majukumu yafuatayo:

  • Kupanga, kuratibu, kudhibiti na kutathmini huduma za uzalishaji wa tumbaku ikiwa ni pamoja na: utaratibu wa kilimo, Usajili wa wakulima, kukuza uzalishaji, Makisio ya uzalishaji, Mfumo wa usambazaji wa pembejeo, Miundombinu ya uzalishaji, Programu ya upandaji miti, Kushiriki maonesho ya wakulima, Utafiti wa zao la tumbaku na huduma za ugani;
  • Kupanga, kuratibu, kusimamia na kutathmini huduma za masoko, utafiti wa masoko na taarifa za masoko, taratibu za uuzaji wa tumbaku ya shambani ndani ya nchi na taratibu za uuzaji wa tumbaku nje ya nchi;
  • Kupanga na kusimamia huduma za kudhibiti ubora wa tumbaku ikiwa ni pamoja na huduma za ukaguzi;
  • Kuimarisha uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya tumbaku katika uzalishaji, usindikaji na ngazi ya masoko ya tumbaku;
  • Kuhakiki na kuchunguza pembejeo ili kuthibitisha kama zinakidhi viwango vilivyothibitishwa;
  • Kuandaa na kutekeleza sera za kurugenzi kwa ajili ya uendeshaji bora wa kurugenzi na kufanikisha malengo yaliyowekwa na kuhakikisha kuwa kurugenzi inafanya kazi ndani ya bajeti ya matumizi ya iliyoidhinishwa;
  • Kushiriki katika utekelezaji wa mpango mkakati wa Bodi;
  • Kumshauri Mkurugenzi Mkuu juu ya masuala yote yanayohusiana na sekta ya tumbaku na kupendekeza mipango mikubwa ya sera;