I. Tumbaku ya Mvuke

fcvTumbaku ya mvuke pia inajulikana kama "Bright" na "Virginia" kwa jina la kibiashara katika soko la dunia. Aina hii ya tumbaku hutumika zaidi katika utengenezaji wa sigara. Baadhi ya majani yake mazito yanaweza kutumika katika mchanganyiko kwa ajili ya kuvuta.

Jani la tumbaku ya mvuke lina sifa ya

  1. kuwa na kiwango cha juu cha sukari:
  2. uwiano wa nitrojeni. Uwiano huu huwa bora kwa kuchuma jani katika hatua ya juu ya kupevuka, na kwa njia ya kipekee ya kukausha ambayo inaruhusu mabadiliko fulani ya kikemikali kutokea katika jani.

Rangi ya majani yaliyokaushwa ya tumbaku ya mvuke hutofautiana kutoka rangi ya ndimu na machungwa hadi mahogany. Majani yake ni makubwa kiasi na huwa makubwa zaidi katika hatua ya kati ya kikonyo. Mmea uliopandwa vizuri huwa katika urefu wa inchi kati ya 39-51 na majani kati ya 18-22 yanayoweza kuvunwa. Majani huvunwa kama vifikie kutoka chini kwenda juu.

Tumbaku ya mvuke hulimwa katika nchi takriban 75 ikiwemo Tanzania.

II. Tumbaku ya Moshi

dfcMatumizi makuu ya tumbaku ya moshi ni katika uzalishaji wa ugoro, tumbaku ya kutafuna, na misokoto. Majani ya tumbaku ya moshi hufukizwa moshi wa kuni katika hatua za awali za ukaushaji. Aina ya miti inayotumika kukausha aina hii ya tumbaku ni muhimu katika kuamua ladha yake.

Majani ya tumbaku ya moshi yaliyokaushwa huwa na rangi iliyokolea na ni mrefu na mazito. 

Wazalishaji wakuu wa tumbaku ya moshi ni Marekani, Poland, Malawi, Italia na Tanzania.