Historia ya kilimo cha tumbaku nchini Tanzania inakwenda nyuma mwanzoni mwa miaka 1960. Ukiacha mkoa wa Songea unaolima tumbaku ya moshi (DFC), mikoa mingine iliyobaki inalima tumbaku ya mvuke (FCV). Mkoa wa Mara kwa kiasi kikubwa unalima tumbaku ya mvuke katika wilaya za Tarime, Serengeti na Rorya. Kuna kiasi kidogo cha tumbaku ya moshi kinachozalishwa katika maeneo yaliyotengwa. Mkoa wa Morogoro kwa sasa unazalisha tumbaku ya mvuke katika maeneo ya Kilosa (Kimamba, Msowero na Kidonga) na Ulanga. Kwa muhtasari tumbaku hulimwa hapa nchini katika maeneo kama inavyoonekana hapa chini;

Mkoa

Aina ya tumbaku

Tabora

Tumbaku ya Mvuke

Urambo

Tumbaku ya Mvuke

Sikonge

Tumbaku ya Mvuke

Kahama

Tumbaku ya Mvuke

Manyoni

Tumbaku ya Mvuke

Mpanda

Tumbaku ya Mvuke

Kigoma

Tumbaku ya Mvuke

Iringa

Tumbaku ya Mvuke

Chunya

Tumbaku ya Mvuke

Morogoro

Tumbaku ya Mvuke

Mara

Tumbaku ya Mvuke, Tumbaku ya Moshi

Songea

Tumbaku ya Moshi