Kitengo cha Huduma za Sheria
Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kitengo cha Huduma za Sheria inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:
- Kutafsiri nyaraka za kisheria na kuishauri Bodi;
- Kuidhinisha nyaraka za kisheria za Bodi;
- Kupitia hati za Udhamini, mikataba ya makubaliano, mikataba na nyaraka nyingine za kisheria;
- Kutayarisha maelezo ya kisheria na kuiwakilisha Bodi katika mashauri ya kisheria;
- Kuwasiliana na Wakala wa kisheria wa nje katika masuala ya kisheria na kushiriki au kuendesha mashauri ya Bodi;
- Kupitia na kuandaa marekebisho ya Sheria ya Sekta ya Tumbaku na kanuni zake;
- Kudumisha ulinzi salama wa nyaraka za kisheria za Bodi;
- Kupanga na kuitisha kikao cha Bodi ya Wakurugenzi;
- Kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya vikao vya Bodi ya Wakurugenzi;
- Kuwa Katibu wa vikao vya Uongozi wa Bodi; na
- Kuandika kumbukumbu wakati wa vikao vya Bodi ya Wakurugenzi na vile vya Uongozi wa Bodi.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:
- Kufuatilia na kupitia taratibu na udhibiti wa uendeshaji wa Bodi;
- Kushauri juu ya utekelezaji wa taarifa ya Mkaguzi wa Nje;
- Kusimamia utayarishaji wa taarifa za ukaguzi wa ndani;
- Kuandaa na kubuni taratibu/mifumo ya ukaguzi;
- Kufanya mapitio ya sera za udhibiti wa ndani ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa bajeti;
- Kusimamia uzingatiaji wa Kanuni za Fedha na Utumishi;
- Kusimamia ukaguzi wa ndani wa mara kwa mara na maalum; na
- Kuwezesha Ukaguzi wa Nje;
Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:
- Kushauri Uongozi juu ya masuala yanayohusiana na ununuzi, vifaa na uhifadhi;
- Kusimamia ununuzi na uhifadhi wa mitambo/vifaa vya Bodi na vifaa vya ofisi;
- Kusimamia uzingatiaji wa sheria za manunuzi ya umma;
- Kusimamia uchambuzi wa orodha ya mali na uhakiki wa hifadhi ya vifaa/mali za Bodi; na
- Kuandaa mpango wa manunuzi wa mwaka.
Kitengo cha Uhusiano wa Umma
Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kitengo cha Uhusiano wa Umma inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:
- Kutayarisha mkakati wa uhusiano wa umma wa Bodi;
- Kuratibu utayarishaji wa taarifa za Bodi zitakazotolewa kwa vyombo vya habari na umma kwa ujumla;
- Kutayarisha majibu ya maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari;
- Kuhariri matangazo na matamko kwa ajili ya kuchapishwa kwenye vyombo vya habari;
- Kuratibu uchapishaji wa jarida la Bodi; na
- Kutoa huduma za itifaki katika hafla zinazoandaliwa na Bodi.