Bodi ya Tumbaku Tanzania ni chombo cha udhibiti wa zao la tumbaku kilichoanzishwa chini ya sheria ya sekta ya  tumbaku Na. 24 ya 2001 (kama ilivyorekebishwa na sheria ya mazao (marekebisho mchanganyiko) Na. 20 ya 2009). Majukumu makuu ya udhibiti ya Bodi kama ilivyoamuliwa katika sehemu ya tano (5) ya sheria ya tumbaku ni:-

  • Uundaji, utekelezaji na uhimizaji wa miongozo ya sera na viwango kwa lengo la kusimamia na kuboresha utendaji wa sekta ya tumbaku nchini Tanzania;
  • Utoaji wa ushauri kwa Waziri anayehusika na kilimo na serikali kwa ujumla juu ya mambo yote yanayohusiana na sekta ya tumbaku; na
  • Uhamasishaji na uendelezaji wa mazingira mazuri kwa ajili ya ufanisi na ushindani kwa wadau wote katika sekta ya tumbaku.

Dira

Kuwa bora katika utoaji wa huduma za udhibiti, ushauri na ukuzaji wa sekta ya tumbaku

Dhamira

Kutoa huduma kwa wakati na ubora kwa wakulima na wafanyabiashara wa tumbaku katika suala la usajili, ushauri wa kitaalam na uwezeshaji wa mchango wa sekta binafsi katika sekta ya tumbaku kwa ukuaji bora na endelevu kwa manufaa ya sekta na nchi.