Matangazo
Tangazo la kushiriki Mkutano wa 23 wa Watendaji wa masoko ya tumbaku kitaifa – 2026
Bodi ya Tumbaku Tanzania inawakaribisha wadau wote wa sekta ndogo ya tumbaku kujisajili kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Mafunzo na Semina Serikalini (TSMS) ili kushiriki katika Mkutano wa 23 wa Wadau wa Masoko ya Tumbaku Kitaifa – 2026. Mkutano huu unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 Aprili, 2026 katika mji wa Singida, Tanzania.
Mkutano huu utawakutanisha wadau mbalimbali, wakiwemo: Wataalam wa masoko ya tumbaku kutoka Bodi ya Tumbaku Tanzania, Makampuni yanayonunua tumbaku, Wakulima wa tumbaku kupitia Vyama vyao vya Msingi, Vyama Vikuu vya Ushirika, Maafisa Ushirika kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo yanayozalisha tumbaku, na Wadau wengine muhimu wa sekta ya tumbaku.
Mkutano huu utatoa jukwaa la kujadili fursa, changamoto na mwelekeo wa kimkakati wa sekta ya tumbaku kabla ya kuanza msimu wa masoko wa 2026/2027.
Mwisho wa kujisajili ni tarehe 10 Aprili, 2026 saa 5:59 usiku. Tafadhali tembelea kiungo https://tsms.gov.go.tz kujisajili.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Bodi ya Tumbaku Tanzania.