Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Bodi ya Tumbaku Tanzania

Matangazo


Zoezi la tathimini ya zao shambani (Crop Survey) kwa msimu wa kilimo 2025 - 2026


Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Bw. Stanley Mnozya anapenda kuwatangazia wadau wa sekta ndogo ya tumbaku nchini kuwa kwa mujibu wa kalenda ya zao la tumbaku, zoezi la tathimini ya wingi na ubora wa zao la tumbaku shambani linaendelea. Zoezi hii lilianza tarehe 09 Februari 2026 na linatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 31 Machi 2026.

Umuhimu wa zoezi hii ni kupata matarajio sahihi ya uzalishaji wa tumbaku kwa kujua wingi na ubora wa zao shambani. Tathimini hii inawapa wadau fursa ya kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya ununuzi wa tumbaku (masoko) kulingana na matarajio hayo.

Bw. Mnozya amewasisitiza wadau wote kushirikiana na maafisa wa Bodi ya Tumbaku Tanzania wanaosimamia zoezi hili katika maeneo yote ya uzalishaji nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha tathimini inafanyika kwa ufanisi. Amesisitiza kuwa ni muhimu kuchukua taarifa sahihi na kwa wakati ili kusaidia katika upatikanaji wa takwimu zilizo sahihi.