Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Tumbaku Tanzania

Kurugenzi

Kurugenzi ya Uendelezaji Zao na Huduma za Udhibiti

Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kurugenzi ya Uendelezaji Zao na Huduma za Udhibiti inatekeleza majukumu yafuatayo:

 1. Kupanga, kuratibu, kudhibiti na kutathmini huduma za uzalishaji wa tumbaku kama vile utaratibu wa Kilimo; Usajili wa mkulima; Kukuza zao; Makadirio ya uzalishaji; Mbinu za usambazaji wa pembejeo; Miundombinu ya uzalishaji; Programu ya Upandaji miti; Siku/mashindano ya wakulima; Uanzishaji na usimamizi wa Mfuko wa Maendeleo ya zao; Utafiti wa zao na huduma za ugani.
 2. Kupanga, kuratibu, kusimamia na kutathmini huduma za masoko, utafiti na taarifa za masoko, taratibu za kuuza tumbaku mbichi na taratibu za kuuza tumbaku ndani na nje ya nchi.
 3. Kupanga na kusimamia huduma za udhibiti wa ubora wa zao ikijumuisha huduma za ukaguzi.
 4. Kuimarisha uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya tumbaku katika ngazi ya uzalishaji, usindikaji, ukuzaji na uuzaji.
 5. Kuthibitisha na kukagua pembejeo ili kuhakikisha uzingatiaji wa viwango vilivyoidhinishwa.
 6. Kutayarisha na kutekeleza sera za Kurugenzi kwa ajili ya uendeshaji bora wa Kurugenzi na kufikia malengo yaliyowekwa na kuhakikisha kuwa Kurugenzi inafanya kazi ndani ya bajeti ya matumizi iliyoidhinishwa;
 7. Kushiriki katika utekelezaji wa mipango mkakati ya Bodi; na
 8. Kumshauri Mkurugenzi Mkuu kuhusu masuala yote yanayohusu tasnia ya tumbaku na kupendekeza mipango mikuu ya kisera.

Kurugenzi ya Fedha

Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kurugenzi ya Fedha inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:

 1. Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika masuala yanayohusu Mipango na Usimamizi wa Fedha na matumizi ya Bodi;
 2. Kusimamia uendeshaji wa shughuli za kifedha za Bodi;
 3. Kuimarisha usimamizi wa fedha na hesabu;
 4. Kufanya majumuisho ya bajeti ya mwaka ya Bodi ya matumizi (OC) na Mishahara (PE);
 5. Kuelekeza na kusimamia utayarishaji wa taarifa za fedha za mara kwa mara;
 6. Kuimarisha matumizi bora ya mapato ya Bodi katika ununuzi na utoaji wa huduma na vifaa;
 7. Kufuatilia upatikanaji wa fedha kutoka katika vyombo husika na kusimamia bajeti ya matumizi ya Bodi na kila idara; na
 8. Kuwezesha ukaguzi wa taarifa za fedha za Bodi.

Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala

Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:

 1. Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika masuala yanayohusu utawala na Mipango na Maendeleo ya Rasilimali Watu;
 2. Kusimamia kumbukumbu sahihi za rasilimali watu;
 3. Kusimamia utayarishaji na utekelezaji wa Bajeti ya Mishahara (PE);
 4. Kusimamia utayarishaji wa taarifa za Rasilimali watu na utawala;
 5. Kusimamia ajira, uteuzi na upandishaji vyeo kwa wafanyakazi wa Bodi;);
 6. Kusimamia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Nyaraka za Kiutumishi;
 7. Kusimamia mikataba ya watoa huduma;
 8. Kusimamia majengo ya ofisi, vifaa na matengenezo yake;
 9. Kuhakikisha kuwa makato ya kisheria ya wafanyakazi yanalipwa.
 10. Kusimamia ustawi wa wafanyakazi (ujira, mishahara na marupurupu mengine);
 11. Kusimamia Tathmini ya Mahitaji ya Mafunzo na maandalizi ya Mpango wa Mafunzo.

Kurugenzi ya Udhibiti Ubora na Masoko

Ili kukuza na kudhibiti tasnia ya tumbaku nchini, Bodi ya Tumbaku Tanzania kupitia Kurugenzi ya Udhibiti Ubora na Masoko inatekeleza majukumu na wajibu ufuatao:

 1. Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika masuala yote yanayohusu ubora na masoko ya tumbaku;
 2. Kuwasiliana na nchi nyingine za kigeni zinazozalisha tumbaku kama nguvu ya pamoja ya kujadiliana bei katika meza ya mazungumzo;
 3. Kusimamia shughuli za utangazaji wa tumbaku ndani na nje ya nchi;
 4. Kuratibu, kudhibiti na kutathmini masoko ya tumbaku ikiwa ni pamoja na utafiti na huduma za ugani;
 5. Kupanga, kuratibu, na kusimamia utafiti wa masoko na utaratibu wa uuzaji wa tumbaku mbichi;
 6. Kutunga sheria na kanuni za udhibiti na uhakiki wa ubora; na
 7. Kusimamia uzingatiaji wa sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya tumbaku katika masoko katika ngazi zote.