Ugani unahusisha utoaji maarifa kwa wa wakulima, taarifa, uzoefu na teknolojia inayohitajika ili kuongeza na kudumisha tija na kwa ajili ya kuboresha ustawi na maisha ya wakulima.
Bodi ya tumbaku Tanzania ina maofisa wa uendelezaji zao wenye ujuzi mzuri ambao hutoa maarifa, taarifa, uzoefu na teknolojia kwa wakulima wa tumbaku waliotawanyika kote nchini. Ili kuboresha utendaji mzuri wa sekta ya tumbaku nchini, Bodi hutumia njia ya mafunzo na kutembelea mashamba, huduma za ugani shirikishi kutoa maarifa yaliyokusudiwa kwa wakulima wa tumbaku.