Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Tumbaku Tanzania

Leseni na Vibali

Utoaji wa Leseni na Vibali

Kwa mujibu wa kifungu husika cha Sheria ya sekta ya tumbaku, Bodi ya Tumbaku Tanzania inaweza kutoa leseni na vibali vifuatavyo kwa watu au kampuni iliyosajiliwa:

 1. Leseni ya Kununua Tumbaku Mbichi Shambani
 2. Leseni ya Kuingiza Tumbaku Mbichi Nchini
 3. Leseni ya Kusindika Tumbaku
 4. Leseni ya Kununua Tumbaku Iliyosindikwa
 5. Leseni ya Kuuza Tumbaku Iliyosindikwa
 6. Leseni ya Kusafirisha Tumbaku Nje ya Nchi
 7. Kibali cha Kuingiza Tumbaku Nchini
 8. Kibali cha Kusafirisha Tumbaku Nje ya Nchi

Jinsi ya Kuomba Leseni na Vibali

Kampuni au mtu anayetaka kununua, kuuza, kusindika, kuingiza au kusafirisha tumbaku nje ya nchi anapaswa kuomba leseni au / na kibali Bodi ya Tumbaku kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa kutoa leseni na vibali (ATMIS) kwa kutembelea kiungo hiki: ATMIS au kwa kutembelea tovuti ya Bodi na kubonyeza kiungo ATMIS.

Mahitaji kwa ajili ya Kuomba Leseni na Vibali

Leseni ya Kununua Tumbaku Mbichi Shambani

Ili kuomba leseni hii nyaraka zifuatazo zinahitajika:'

 1. Mkataba kati ya wakulima na mnunuzi Kivuli
 2. Uthibitisho wa kutoka benki au mfadhili
 3. Mkataba kati ya mununuzi na kiwanda Kivuli
 4. Orodha ya bei ya madaraja ya tumbaku

Leseni ya Kununua Tumbaku Iliyosindikwa

Ili kuomba leseni hii nyaraka zifuatazo zinahitajika:

 1. Hati ya usajili wa Kampuni
 2. Leseni halali ya Biashara
 3. Hati ya utambulisho wa mlipa kodi
 4. Uthibitisho kutoka benki ya mteja

Leseni ya Kuuza Tumbaku Iliyosindikwa

Ili kuomba leseni hii nyaraka zifuatazo zinahitajika:

 1. Hati ya usajili wa Kampuni
 2. Leseni halali ya Biashara
 3. Uthibitisho kutoka benki ya mteja

Leseni ya Kusindika Tumbaku

Ili kuomba leseni hii nyaraka zifuatazo zinahitajika:

 1. Orodha ya wakurugenzi/washirika wa kampuni na hisa wanazomiliki
 2. Leseni halali ya Biashara
 3. Leseni ya Viwanda

Kibali cha Kusafirisha Tumbaku Nje ya Nchi

Ili kuomba kibali hiki nyaraka zifuatazo zinahitajika:

 1. Maelezo ya usafirishaji wa shehena
 2. Taarifa ya upakiaji iliyotiwa saini / kuidhinishwa
 3. Mchanganuo wa bei ya kila daraja kwa tumbaku inayouzwa nje ya nchi
 4. Ankara ya tumbaku inayosafirishwa (kivuli)

Kibali cha Kuingiza Tumbaku Nchini

Ili kuomba kibali hiki nyaraka zifuatazo zinahitajika:

 1. Hati ya utambulisho wa mlipa kodi
 2. Hati ya usajili wa Kampuni
 3. Hati ya usajili wa biashara / kampuni
 4. Leseni ya Biashara
 5. Uthibitisho kutoka benki ya mteja

Mambo yanayoweza kuifanya Bodi kukataa kutoa leseni kwa mwombaji

Bodi inaweza kukataa kutoa leseni kwa mwombaji ambaye:-

 1. Ameshindwa kuonyesha ushahidi wa uwezo wa kufanya biashara zinazohusiana na leseni anayoomba;
 2. Kwa mtizamo wa Bodi, mwombaji hawezi kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni;
 3. Anadaiwa na Bodi, mkulima, mnunuzi au msindikaji; au
 4. Ameshindwa kuzingatia vigezo na masharti yanayohusiana na leseni iliyotolewa kwake katika msimu uliopita.

Kusimamishwa na Kufutwa kwa Leseni

 1. Bodi, kwa sababu maalumu zinazojulikana kwa mmiliki wa leseni iliyotolewa, inaweza kusimamisha au kufuta leseni.
 2. Mtu / kampuni, ambayo leseni yake imesimamishwa au kufutwa na Bodi, haitafanya miamala yoyote ya kibiashara inayohusina na leseni hiyo katika kipindi cha kusimamishwa au kufutwa.
 3. Mara tu mmiliki wa leseni atakapo rekebisha tatizo lililolazimisha kusimamishwa kwa leseni na baada ya kuisha kwa katazo lililowekwa, Bodi itasitisha kusimamishwa kwa leseni husika.